Hapa takeer.com, tuna fanya projects kibao zingine ni just for fun! Tumetengeneza namna itakayokuwezesha kutoa msaada kwa watumiaji au watembeleaji wa mtandao/blogu yako na kupata maoni kirahisi kutoka kwa watumiaji wa mtandao.

Ingekuwa rahisi hata wewe mwenyewe kufanya, ila tumerahisisha zaidi kwa kukuwezesha kuweka mtandao zaidi ya mmoja na kila mtandao unaweza kuchagua rangi na vingine vingi ili kuendana na mtandao wako husika.

Uzuri wa tulichokiteneza, kitafanya kwenye aina ya mtandao(website) yeyote. Iwe blogspot, wordpress au mtandao uliotengenezwa pasipo kutumia wordpress au joomla au vingine.

Namna ya Kujiunga

Kujiunga ni rahisi, wala huhitaji kuingiza taarifa zozote, unachotakiwa kuwa nacho ni account ya gmail ambayo na yenyewe hutaiingiza, itakuhitaji kubonyeza get started halafu itakupeleka kwenye kuchagua email utakayoitumia kwa mitandao utakayoiweka kwenye wasupport.takeer.com. Ukishachagua email itakuingiza moja kwa moja ndani na kuanza kuweka mtandao unaotaka kuweka whatsapp support.

Baada ya kuingia, utaweka anwani ya mtandao na baada ya kutuma, mtandao uliouweka utaonekana chini, ukibonyeza huo mtandao utakupeleka kwenye kuweka taarifa za mtu au group la whatsapp litakalokuwa linapokea jumbe za watakaotembelea mtandao/blogu yako.

Pia itakuwa na sehemu imeandikwa widget setup, ambapo utaweza kuchagua rangi ya widget yako na maneno unayotaka yaonekane kwenye widget ya website/blogu yako husika. Pia utaweza kuona code ambazo unatakiwa uzinakili(copy) na kwenda kuziweka kwenye mtandao/blog yako.

Namna ya kuziweka kwenye website/blogu

Kama unatumia wordpress, inakubidi uingie kama admin na uangalie kama theme unayotumia ina sehemu itakayokuwezesha kuweka custom codes kwenye footer. ukiipata right click na paste code ulizozicopy kwenye wasupport.takeer.com na u update au save. Ukitembelea blog yako, utaona ki button cha whatsapp chini na ukikibonyeza kitatanuka na kuonesha taarifa zaidi. Utakuwa umeweza kuweka kwenye blogu yako.

Kama hutumii wordpress, cha msingi ni ku weka code ulizozicopy kabla ya kufungwa </body> kwenye website yako.

Wasiliana nasi endapo utakwama kupitia kibutton cha whatsapp hapa chini.